Wednesday , 10th Sep , 2014

Msanii mkali wa muziki wa Bongofleva, Timbulo amesema kuwa kuna tatizo kubwa la Menejimenti za wasanii wengi hapa nchini Tanzania kutojituma zaidi kuandaa shoo kwa wasanii wao, ili kuwainua zaidi kimapato.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini Timbulo

Msanii huyu amesema kuwa, kwa upande wake binafsi sasa ameanza kusafiri sehemu mbalimbali na kufanya maonyesho kama njia ya kujikwamua, akiwa pia ameanza kutoka nje ya mipaka ya nchi, ingawa kuna changamoto ya msanii akiwa peke yake kuandaa kila kitu mwenyewe.