Monday , 26th Aug , 2019

Baada ya kushikiliwa kwa zaidi ya masaa 48 katika kituo cha polisi cha Chang'ombe, viongozi watatu wa ACT - Wazalendo, akiwemo Katibu wa Kamati ya Uadilifu, Mbarala Maharagande na mwandishi wa habari wa Gillybony TV, Haruna Mapunda, hatimaye leo Agosti 26 wamepatiwa dhamana.

Viongozi hao pamoja na mwanahabari huyo,  walikamatwa siku ya Agosti 24,

Wakati wa shughuli ya ufunguzi wa matawi na kikao cha ndani katika Kata ya Azimio Jimbo la Temeke Dar es Salaam, kwa madai ya kuwa walifanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Dhamana hiyo imepatikana kwa msaada wa Mawakili kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), wakiongozwa na Boniface Mapunda, George Masoud, Catherine Ringo pamoja na Shilinde Swedy.