Monday , 26th Aug , 2019

leo Agosti 26, 2019, Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi ametangaza Baraza la Mawaziri, baada ya kukaa miezi 7 tangu achaguliwe kuwa Rais wa nchi hiyo, bila ya kuwa na baraza.

Katika baraza hilo imeelezwa idadi ya wanawake ni ndogo zaidi ambayo ni asilimia 17, na wanaume wakiongoza kwa asilimia 83, huku baadhi ya wachambuzi wa siasa Mjini Kinshasa wakisema kuna sura mpya.

Serikali hatimaye imewadia Rais amesaini agizo rasmi na tutaanza kufanya kazi hivi karibuni.” Waziri Mkuu Sylvestre Ilunga.

Mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais wa DR Congo, Julai mwaka huu Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi na aliingia kwenye makubaliano na mtangulizi wake Joseph Kabila juu ya kuundwa kwa Serikali ya Muungano. ambapo katika Baraza hilo Chama Cha Kabila kimepata Mawaziri 43, na cha Thikesedi kimepata Mawaziri 23.