Aliyekuwa mtangazaji wa DW, Mohamed Dahman
Taarifa hizo zimetolewa na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt, akisema kuwa Dahman alikuwa ni mwandishi bora na alipendelea sana kusoma taarifa ya habari za ulimwengu na makala ya mbiu ya mnyonge.
Aidha taarifa hiyo imebainisha kuwa, Dahman alikuwa akiugua kwa kipindi cha takribani miaka miwili na muda wote huo hakuweza kufanyakazi. DW imepeleka pole za dhati kwa mke wake, binti yake na familia yake visiwani Zanzibar na ughaibuni.

