
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Frolence Ikorongo amesema Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kujiridhisha bila shaka, kwa kutumia ushahidi wa upande wa mlalamikaji, na kutupilia mbali utetezi wa Baba levo.
Awali Mahakama ilitoa uamuzi wa mshtakiwa Baba Levo, kwenda jela mwaka 1 ndipo akajitetea kwa kuiomba Mahakama impunguzie adhabu, kwani anategemewa na watoto 4 pamoja na wananchi zaidi ya 25000.
Baba Levo ameendelea kujitetea kuwa endapo atafungwa mwaka 1 atapoteza sifa za kuendelea kuwa Diwani, hivyo ataisababishia Serikali hasara ya kufanya uchaguzi upya, na kwamba ni mara ya kwanza kukutwa na kosa la shambulio
Baada ya Hakimu kusikiliza utetezi huo akaamua kupunguza adhabu na kuamuru kwenda jela miezi 5, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo