Thursday , 1st Aug , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amezindua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jengo la tatu (Terminal 3), jijini Dar es salaam mradi ambao unagharimu zaidi ya Bilioni 720.

Akizuzumgumza kwenye uzinduzi huo, Rais Magufuli amesema licha ya Serikali yake kutekeleza mradi huo, lakini hadhani kama watakaomtangulia kwenye nafasi hiyo ya Urais wataweza kuyatimiza anayoyafanya, kwa kile alichokieleza amekuwa akisemwa mara kwa mara.

"Saa nyingine najiuliza kweli tumeweza? mimi siwezi kusimama mbele ya watu nikasema haya ni kwa sababu yangu, mimi ni dereva tu, najiuliza siku Mungu akanichukua, wanaokuja wataweza  kuyamaliza, kwa sababu unafanya hivi huku unatukanwa." amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema kuwa "jengo hili lmegharimu mabilioni ya fedha zaidi ya bilioni 700, fedha hizi zimetolewa na Watanzania kwa asilimia 100, ambapo asilimia 15 fedha taslimu na 85% tumekopa , na mkopo huu utarejeshwa kupitia kodi zetu."

Kwa mara ya kwanza mradi huo wa Uwanja wa Ndege ulianza mwaka 2013, lengo lake ni kuongeza idadi ya watumiaji wa usafiri wa anga, ambapo kwa sasa kupitia Terminal 1, 2, 3 zaidi ya abiria Milioni 8 kwa mwaka watatumia.