
masuala ya kiuchumi.
Hati hizo za makubaliano zimesainiwa Harare Zimbabwe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi, kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Zimbabwe Luten Jenerali Mstaafu Sibusiso Moyo.
Akizungumza mara baada ya kusaini hati hizo za makubaliano Waziri Kabudi amesema mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 21,. na kuongeza kuwa uhusiano baina ya Tanzania na Zimbabwe ulianza kabla ya ukoloni.
Makubaliano hayo yameafikiwa katika nyanja za ushirikiano wa biashara, uchumi na uwekezaji, siasa na diplomasia, utalii, uwezeshaji wa wanawake na masuala ya jinsia pamoja na masuala.