Friday , 26th Jul , 2019

Msanii wa kike wa muziki wa BongoFleva Mwasiti, amefunguka kuhusu gharama anazotumia kwenye suala zima la mavazi pamoja na kutofanya kazi na wasanii wa kike.

Mwasiti amefunguka hayo leo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kuhusu anatumia kiasi gani cha pesa kwenye suala la mavazi.

"Mimi sifikishi hata Laki, kuna mavazi mengine yanakuwa ya gharama sana na mavazi mengine ni ya kawaida tu kama hivi nilivyo leo huwezi kumaliza hata Laki, napenda sana kuvaa kawaida kabisa, nikivaa vazi ambalo halina 'hills' nakuwa vizuri kabisa kabisa".

Aidha msanii huyo amesema kwamba anawapenda wasanii wa kiume kwa sababu wana uharaka kwenye ufanyaji kazi na wanakuwa hawana usumbufu wowote, pia anakuwa vizuri zaidi akifanya kazi na wasanii wa kiume kuliko wa kike, kwa sababu wasanii wengi wa kike wana mazoea na wanakuwa hawana umakini.

Mwasiti tayari ameshafanya kazi na wasanii wengi wa kiume kama Chid Benz, Godzilla, Roma, Billnass na G nako