Friday , 5th Sep , 2014

Takribani watu zaidi ya 36 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 79 kujeruhiwa baada ya magari mawili ya abiria kugongana uso kwa uso katika eneo la Sabasaba wilayani Butiama, mkoani Mara leo asubuhi.

Watu 36  wamefariki  dunia  papohapo  na wengine 79  kujerihiwa vibaya  katika  ajali  mbaya  ambayo imetokea Saa Tano leo Asubuhi  katika  kijiji cha  Sabasaba nje kidogo ya mji wa Musoma  wilaya  ya Butiama  mkoani mara kwa kuhusisha mabasi  mawili  ya  abiria  na  gari  dogo aina  ya  Nissani  Tellono  yenye  namba  za usajili T332 AKK
  
Mbali   na  gari  hilo   kugongwa na  kutumbukia  ndani  ya  mto  mmoja  katika  daraja  hilo  kwenye barabara kuu  ya Musoma–Mwanza  pia   mabasi  mawili  ambayo  yamehusika  katika  ajali  mbaya ni  J4 Express  yenye namba za usali  T677CYC liyokuwa ikitokea jijini  mwanza kwenda Sirari  wilayani  Tarime   ambalo  limegongano uso  kwa uso  na  basi  la  Mwanza  coach   yenye  namba tT736  AWJ  lilokuwa likitokea  Musoma kwenda  jijini Mwanza.
 
Baada  ya  taarifa  za  ajali  kusambaa  katika manipaa ya  musoma  vilio   na  simanzi  vimetawala  katika  mji huo wa musoma mkoani  mara  baada majeruhi   na  miili   ya  marehemu   wa  ajali  hiyo  kuanza kufikishwa  katika  hospitali  ya rufaa ya  mkoa wa Mara  mjini  Musoma
 
Wakizungumza wakati  wakipatiwa matibabu  baadhi  ya  majeruhi  wa ajali hiyo   wamesema  kuwa  ajali hiyo imesababishwa  na  mwendo  kasi  wa mabasi   hayo  hatua ambayo ilisababisha kushindwa kupishana katika daraja hilo hivyo  kugongana uso kwa uso.
 
Akizungumza  kwa niaba  ya  mganga mkuu  wa  mkoa wa  Mara DKT Martin Khan, amesema  kuwa wamepokea maiti na idadi kubwa ya majeruhi  na wengi  wao hali  zao  si za kuridhisha.
 
Hata hivyo  DKT  Khan  ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujitolea damu kwani amesema kuwa hospital  hiyo ya  rufaa  ya  mkoa wa  mara inakabiliwa na upungufu mkubwa wa damu katika kuhudimia wagonjwa wakiwemo majeruhi wa ajali…
 
Kamanda wa polisi mkoa wa  Mara ACP Alex Kalangi, akizungumza na EATV kwa njia  ya simu amethibitisha kutokea kwa  ajali  hiyo  na kwamba taarifa  rasmi  za jeshi  la polisi  zitatolewa baada ya kupata  taarifa  kutoka kwa madaktari na  kwamba ametoa wito kwa  wananchi kujitokeza  katika  hospitali  ya  mkoa  kwaajili  ya kutambua  miili  ya  marehemu.