Friday , 7th Mar , 2014

Waumini wa msikiti wa Masjidi Quba uliopo eneo la Makao Mapya Mkoani Arusha wameswali swala ya Ij

Waumini wa msikiti wa Masjidi Quba uliopo eneo la Makao Mapya Mkoani Arusha wameswali swala ya Ijumaa hii leo chini ya ulinzi mkali wa Polisi, ambao waliuzunguka msikiti huo wakiwa na silaha.

Aidha kabla ya polisi kuuzunguka msikiti huo, Maimamu wawili Japhali Lema na Hassan Waziri walichukuliwa na polisi hadi kituo cha Polisi Makao Makuu mjini Arusha kwa mahojiano kutokana na majibizano makali baina yao kuhusu nafasi ya kuongoza msikiti huo.

Muumini wa msikiti huo Ally Shemdoe amesema chanzo cha polisi kujaa msikitini hapo ni kutoelewana baina ya Imamu aliyekuwa akiongoza msikiti huo awali Japhali Lema, ambaye kwa sasa amesimamishwa uongozi na Bakwata na kuwekwa Imamu Hassani Waziri.

Kwa upande wake Imamu aliyeongoza swala ya Ijumaa katika msikiti huo, Mohamed Hambari, amesisitiza umuhimu wa Waislamu kuendeleza amani wakati wote na kuwaasa kuepukana na vurugu.