Thursday , 28th Mar , 2019

Mbunge wa Bunda mjini, Esther Bulaya amesababisha kuahirishwa kwa kesi inayomkabili yeye pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA kutokana na kutofika mahakamani.

Esther Bulaya

Leo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilikuwa ikisubiri mashahidi wa Upande wa Jamhuri kwa ajili ya kesi hiyo Na. 112/2018.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi 16/4/2019 kutokana na kwamba Mbunge huyo ni mgonjwa hivyo kushindwa kuhudhuria mahakamani hapo.

Bulaya na Viongozi wengine saba wa wa CHADEMA wanatuhumiwa kwa kosa kufanya maandamano haramu yaliyopelekea kifo cha mwanafunzi wa Akwilina, mwanzoni mwa mwaka uliopita.