
Kibao cha Mahakama kuu.
Jaji Kiongozi wa mahakama hiyo Dr. Eliezer Feleshi ametoa amri hiyo baada ya wakili wa Mkundi kuiambia mahakama kuwa tayari nafasi ya mteja wake imetangazwa kujazwa kwenye uchaguzi wa mwezi Februari mwakani.
Kesi ya kuomba kutengua maamuzi ya kumfungia mkundi yalifungulliwa mwezi Mei mwaka huu na maamuzi ya kesi hiyo yatatolewa tarehe 15 Februari 2019.
Katika kesi hiyo Mkundi aliwakilishwa na Muga na TFF iliwakilishwa na Afisa sheria wake Herman Kidifu.
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemfungia maisha kutojishughulisha na mchezo wa mpira wa miguu Bw. Dunstan Mkundi ambaye alikuwa Msimamizi wa Kituo cha Mtwara.
Mkundi ambaye alikuwa Msimamizi wa michezo ya ligi kuu katika kituo cha Mtwara alifungiwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania kwa kosa la kushindwa kuwasilisha fomu ya mapato ya mchezo kati ya Ndanda FC na Simba uliofanyika Desemba 30, 2017.