Tuesday , 6th Nov , 2018

Baada ya klabu ya Simba kufanikiwa kumaliza uchaguzi wake vizuri na kupata viongozi wapya siku ya Jumapili Novemba 4, 2018, Shirikisho la soka nchini (TFF), limewapongeza viongozi waliochanguliwa.

Kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Simba SC ni Crescentius Magori na kulia ni Rais wa TFF Wallace Karia.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari leo, TFF imepongeza zoezi zima la uchaguzi lilivyokuwa huru na la haki hivyo kuweka wazi kuwa viongozi waliopatika wanatambulika na watapata ushirikiano wote.

''Tunawapongeza viongozi wote waliofanikiwa kuchaguliwa kuiongoza klabu ya Simba, shirikisho lipo tayari kushirikiana nao kwa maendeleo ya mpira wa Tanzania'', imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

@simbasctanzania

A post shared by Tanzania Football Federation (@tanfootball) on

Simba ambayo kwasasa inaongozwa kwa mfumo wa kampuni ilipata viongozi wake wapya ambao wataiongoza kwa miaka 4 wakiwa chini ya Mwenyekiti Swedi Mkwabi pamoja na wajumbe watano.

Wajumbe hao ni Asha Baraka, Hussein Mlinga, Zawadi Kadunda, Seleman Said na Mwina Kaduguda. Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Simba SC ni Crescentius Magori ambaye naye alitangazwa katika mkutano huo.