Tuesday , 6th Nov , 2018

Ubalozi wa Marekani nchini umewaonya raia wake juu ya sakata la kukamatwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Mashoga) na kuwataka kuwa makini pindi wanapotembelea maeneo mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Rais wa Marekani Donald Trump.

Kupitia website yao ubalozi huo wa marekani umewataka raia wake na kuhakikisha wanatoa baadhi ya picha zao ambazo walizichapisha kupitia mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa na viashiria mapenzi ya jinsia moja.

Katika tangazo lao ubalozi huo marekani pia umewataka raia wake kuwa makini na lugha ambazo zitaashiria kuwa ni wahanga vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ili kuepuka uvunjifu wa sheria za Tanzania.

Aidha ubalozi huo umeitaka serikali ya Tanzania kutoa taarifa kama watamkamata moja kati ya raia wa marekani ambaye atatuhumiwa kwa matendo hayo.

Kampeni maalum ya kupambana na mapenzi ya jinsia moja ilianzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda licha baadaye kupitia Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga kusema suala hilo ni mtazamo binafsi wa mkuu huyo mkoa.

Jana katika mkutano wake waandishi wa habari Msemaji wa serikali Dkt Hassan Abbasi alisema “serikali ina mfumo ambao uko wazi, mfumo wa serikali una msemaji katika kila ngazi inapokuwa masuala ya kitaifa ni kati ya msemaji mkuu ni au viuongozi wakuu wa kitaifa pale ambapo kiongozi akitoa tamko kuhusu jambo la kitaifa si tamko la serikali, akitokea katibu kata anazungumzia jambo la kitaifa hilo sio lake