Tuesday , 5th Aug , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Vanessa Mdee, amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa licha ya kufanya show na msanii Jose Chameleone, suala la wao kufanya kazi ya pamoja halikufanyika ila ni kitu ambacho kipo kwenye uwezekano.

msanii Vanessa Mdee wa nchini Tanzania

Vanessa amesema kuwa, katika kushirikiana na msanii, yeye huwa hazingatii kukutana tu na kufanya kazi, bali anazingatia maelewano na kujituma kufanya kitu kizuri kwa pamoja.

Vanessa amepanga pia kushirikiana na wasanii wakubwa hususan kutoka huko Nigeria,
kazi ambazo ni moja ya project zake kubwa kuwahi kuzifanya.