Friday , 1st Aug , 2014

Mchekeshaji nyota wa nchini Kenya Eric Omondi anatarajia kutua kesho nchini Rwanda-Kigali kutumbuiza katika tamasha kubwa litakalowaunganisha nyota wa fani hiyo barani Afrika.

mchekeshaji Eric Omondi wa nchini Kenya

Eric Omondi ameelezea kuwa tamasha hilo lililobatizwa jina 'The Comedy Knights Crew' litajumuisha nyota kutoka nchini Burundi anayejulikana kwa jina Kigingi, Arthur Nkusi, Bubu na Micheal na wengineo wengi..

Lengo la tamasha hilo kubwa ni kuunganisha wachekeshaji hao barani Afrika wanaofahamika kama Stand Up Comedians.