
Bendera ya Tanzania
Majaliwa ameyasema hayo leo Jumapili, Septemba 02 ,2018 wakati akihutubia kongamano la biashara kati ya Tanzania na China kwenye Hoteli ya Winstin jijini Beijing nchini China.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria kwa dhati kujenga uchumi wa viwanda, pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.
"Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika", amesema Majaliwa.
Waziri Majaliwa amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.
"Tanzania inafanya juhudi kubwa ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo mkubwa katika kujenga msingi imara wa viwanda. Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya nje na ukanda maalum wa kiuchumi tukilenga kutimiza mkakakati wetu wa kukuza uchumi wa viwanda na biashara", amesisitiza Majaliwa.
Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji kuanzisha taasisi za kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.
Katika miaka ya hivi karibuni nchi ya Tanzania imekuwa ikipokea wawekezaji wengi kutoka nchi za nje, kutokana na utendaji kazi mzuri wa Rais Dkt. Magufuli pamoja na hamasa zake anazozitoa kwa mabalozi mbalimbali wanaokwenda kuwakilisha taifa nje ya nchi kupigania uwekezaji wa ndani uongezeke nasio kwenda kukaa maofisini tu.