Sunday , 20th Jul , 2014

Mwimbaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bendi maarufu ya muziki wa Taarab nchini Tanzania Mashauzi Classic Modern Taarab, Isha Mashauzi amejiandaa kuwapa zawadi kwa mashabiki wake jijini Dar es Salaam.

mwimbaji wa Taarab nchini Isha Mashauzi

Isha ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa kimya akipika kazi zake amesema kuwa amepanga kutoa albam yake mpya aliyoibatiza jina 'Sura sulambi, Sura si roho, nafsi ya mtu huwezi kuitambua kwa kumwangalia mwake usoni'.

Isha Ramadhan au almaarufu kama Super Woman ameongea na eNewz kuhusiana na albam yake hiyo mpya ambayo ni ya Nne kutoka aliyowashirikisha wanamuziki mbalimbali nchini inayotarajiwa kutoka baada ya mfungo wa mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan.