
Muigizaji wa vichekesho nchini Mzee Majuto
Mzee Majuto amesema hayo leo Juni 22, 2018 akiwa wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere baada ya kuwasili akitokea nchini India, alipokuwa akifanyiwa matibabu ya tezi dume na kuongeza kuwa kuna tofauti ya huduma ya kimatibabu kati ya hapa nchini na alipokuwa India.
“Mimi sijambo nashukuru, Hospitali ni Hospitali isipokuwa wenzetu wapo mbali zaidi, nimefanyiwa mambo mengi sana ambayo kama nisingefanyiwa ningeondoka mapema sana namshukuru Mungu” amesema Majuto.
Mzee Majuto ameongeza kuwa baada ya kumaliza matibabu hayo anataka kutenga muda mwingi kwaajili ya kupumzika zaidi na kuacha kujihusisha na masuala ya sanaa ya uchekeshaji na kudai kuwa Tanzania bado kunawachekeshaji wengi ambao wataweza kuendeleza sanaa hiyo.
Muigizaji huyo wa vichekesho kwasasa amepokelewa na yupo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Mei 4, 2018 Mzee Majuto alisafirishwa kwa gharama za serikali, kwenda nchini India kwa matibabu ya tezi dume baada ya kusumbuliwa na ugonjwa huo kwa kipindi cha muda mrefu.