Saturday , 5th Jul , 2014

Baadhi ya wadau wa elimu nchini Tanzania wamezidi kuupigia kelele mfumo wa elimu Tanzania, huku wakitupia lawama kwa mpangao wa Matokeo Makubwa Sasa kwa kutoweka ushindani unaotakiwa.

Wanafunzi wa moja ya shule zilizopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga nchini Tanzania

Mfumo wa elimu nchini Tanzania umekuwa na changamoto nyingi zikiwemo za ukosefu wa vifaa vya kujifunzia kinadharia kwa wanafunzi huku mpango wa Matokeo Makubwa Sasa BRN ukitajwa kuleta ushindani usio na mwelekeo mzuri kwa wanafunzi

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam Dk. Kitila Mkumbo amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye kongamano la elimu lililoandaliwa na Chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Ardhi Aristide Maulid Nkugu, Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam Marwa Said wakizungumza kabla ya Kongamano hilo wamesema mfumo uliopo umekuwa ukiwaandaa vijana kinadharia zaidi kuliko kufanya kazi kwa vitendo hivyo kuwaandaa kuajiriwa kuliko kujiajiri.