Wednesday , 2nd Jul , 2014

Mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone ameelezea kuwa hivi sasa anajiandaa kutoza kiasi cha dola 400 za kimarekani ambazo ni sawa na shilingi milioni moja za Uganda kwa ajili ya tiketi za watu muhimu yaani VIP kwa ajili ya tamasha lake.

Mwanamuziki Jose Chameleone wa Uganda

Jose Chameleone ambaye alifanya onyesho lake wiki iliyopita jijini humo, amesema kuwa ameamua kutoza kiasi hicho kikubwa kutokana na kwamba anampango wa kufanya tamasha la muziki kubwa na ghali kuwahi kutokea katika historia nchini humo.

Tamasha hilo alilolibatiza jina "One man, One show, One Stage, One million." litafanyika nchini Uganda mwishoni mwa mwaka huu.