Sunday , 18th Feb , 2018

Klabu ya soka ya Simba leo inatarajiwa kuondoka nchini leo kuelekea nchini Djibouti kwaajili ya mchezo wake wa marudiano hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo leo wametangaza kikosi kitakachosafiri.

Kikosi kitakachosafiri leo ni Aishi Salum Manula, na Emanuel Elias Mseja, Mohamed Hussein Mohamed, Mzamiru Yassin Said na Bukaba Paul Bundala. Wengine ni Emmanuel Arnold Okwi, Moses Peter Kitandu na Shiza Ramadhani Yahya.

Wachezaji wengine ni Nicholas Gyan, Erasto Edward Nyoni, James Agyekum Kotei, Shomari Salum Kapombe, Mwinyi Kazimoto Mwitula na Jonas Gellard Mkude, John Raphael Bocco na Ally Shomary Sharifu.

Katika kundi hilo la wachezaji 20 pia wapo wachezaji Said Hamisi Ndemla, Yusufu Seleman Mlipili, Murushid Juuko na Kwasi Asante.

Katika safari hiyo mshambuliaji wa Simba SC John Bocco atakosekana kikosini kutokana na kuwa majeruhi hivyo anaendelea na matibabu na hatasafiri na timu leo jioni.