Monday , 4th Dec , 2017

Waasi wa Kihouthi wanadai kwamba Rais wa zamani wa Yemen, Ali Abdullah Saleh, ameuwawa katika mapigano mjini Sanaa.

Awali kulikuwa na taarifa za kutatanisha kuhusu hali ya Rais Saleh hasa baada ya nyumba yake kushambuliwa kwa bomu na waasi wa Kihouthi ambapo baada ye radio ya waasi hao ilitangaza kwamba ameuwawa.

Picha za mwili wa kiongozi huyo wa zamani zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonesha amekufa..

Wiki iliyopita wafuasi wa Bw. Saleh walikuwa wameungana na waasi wa Kihouthi kupambana na vikosi vya serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia.