Akiongea na mwandishi wa East Africa Television Kamanda wa Polisi Msaidizi Kanda Maalum Benedict Kitalika, amesema moto huo amabo ulitokea leo majira ya saa 3 asubuhi, haujajulikana umesababishwa na nini lakini umeteketeza mali zote zilizomo kwenye nyumba hiyo, ambazo pia thamani yake bado haijajulikana.
Kamanda Kitalika amesema moto huo ambao ulianza katika chumba kimoja anachoishi mpangaji na kisha kusambaa kwenye vyumba vingine na kuteketeza nyumba yote, haujaleta madhara kwa binadamu kwa kutokuwa na taarifa yoyote ya kifo au majeruhi.