Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita mama Anna Makinda alivyokuwa na muda wake kuliongoza bunge hilo.
"Mi nawashangaa, Zitto utapambana na Spika kweli? naweza kukupiga marufuku kuongea humu mpaka miaka yako ikaisha, na hakuna pa kwenda, hakuna cha swali, hakuna cha nyongeza, hakuna cha kuongea chochote humu ndani ya bunge, utanifanya nini? pambana na kitu kingine ila sio Ndugai", amesema Spika Ndugai.
Aidha Spika ameagiza tena Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kumhoji Mbunge huyo kwa kuendelea kutoa kauli za kulidhalilisha Bunge.
Hapo jana Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge