Sunday , 8th Jun , 2014

Msanii mkali wa nchini Nigeria Davido amechaguliwa kuwa mshindi wa tuzo za muziki za Africa Music Awards zilizofanyika nchini Afrika Kusini.

Msanii Davido wa Nigeria

Davido ametwaa tuzo mbili zikiwemo za msanii bora wa kiume na msanii bora wa mwaka ambapo katika sherehe hizo pia kundi la Mafikizolo limetwaa tuzo ya kundi bora la mwaka.

Aidha msanii Tiwa Savage wa nchini Nigeria ametwaa tuzo ya msanii bora wa kike, ambapo Lupita Nyong'o amezidi kung'arisha nyota yake kwa tuzo ya Personality of the Year, huku Ashish J. Thakkar kutoka Tanzania akitwaa tuzo ya Best Leadership Award.