Tuesday , 3rd Jun , 2014

Mfuko wa Bima ya Afya nchini Tanzania umesema changamoto inayoukabili mfuko huo hivi sasa ni jinsi ya kuhakikisha inatoa huduma hiyo kwa kundi la watu wasio na uwezo pamoja na wale wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu.

Aliyewahi kuwa mbunge wa Busega Raphael Chegeni akisalimiana na aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Edward Lowassa.

Mkurugenzi wa Matibabu na Huduma za kifundi wa Mfuko huo Dkt. Frank Lekei, amesema hayo jijini leo Dar es Salaam katika mkutano wa pamoja baina ya NHIF na wachungaji wa KKKT kutoka Dayosisi ya Mashariki na Pwani, mkutano uliolenga kulifahamisha kundi hilo umuhimu na faida za bima ya afya.

Kwa upande wake, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambaye pia ni mjumbe wa bunge maalumu la katiba mchungaji Ernest Kadiva, amewataka waumini wa dini ya Kikristo nchini kujenga utamaduni wa kujifunza na kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu nchi yao ikiwemo mchakato unaoendelea hivi sasa wa kupata katiba mpya.

Kwa mujibu wa mchungaji Kadiva, ufahamu wa Katiba utawawezesha waumini hao kufahamu haki zao za msingi pamoja na mambo mengine muhimu katika maisha yao, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kupata huduma bora za afya.