
George Lwandamina
Lwandamin amesema kocha huyo wa Zanazo kumjua siyo sababu ya kumfunga dimbani, kwa kuwa kila timu inakuwa na muongozo wake wa namna ya ufundishaji na kwamba hata yeye Lwandamina kuijua Zanaco siyo sababu ya kuopata ushindi kirahisi.
"Nashangaa kocha wa Zanaco kudai anajua falsafa za ufundishaji wangu, ila naheshimu mtazamo wake maana ndicho anachokijua ila ninachofahamu mimi falsafa haiwezi kuwa sawa, unapokuwa timu mpya unakuja unakutana na mambo mapya wewe unayaboresha tu". Alisema Lwandamina
Tambo hizo ni kuelekea katika mchezo wa klabu Bingwa Afrika utakaopigwa kesho Jumamosi katika katika dimba la Taifa kati ya Yanga na Zanaco, ambapo Lwandamina ameendelea kusema "Mimi kuwa Mzambia haimaanishi nitaijua kila timu ya Zambia, nafikiri haiwezekani, sijafundisha kila timu Zambia na kama mnavyofahamu nipo Tanzania kwasasa siwezi kuwa Tanzania na wakati huo huo nikawa Zambia". Alisisitiza kocha huyo wa Yanga
Kwa upande mwingine kocha huyo alishindwa kuweka bayana kuhusu baadhi mshambuliaji wake Donald Ngoma kama ataweza kushuka dimbani siku ya kesho dhidi ya hao Zanaco.