Monday , 6th Mar , 2017

Bosi wa lebo ya muziki ya J Entertainment, QS Mhonda amefunguka na kusema atamuomba radhi msanii aliyekuwa chini yake, Q-Chief endapo atabaini kuwa alimkosea msanii huyo.

QS Mhonda ndani ya FNL

Pia QS amemtaka pia Q Chief kufanya hivyo endapo ataona alichokifanya hakikuwa sawa.

Akiongea kupitia kipinid cha FNL kinachorushwa na EATV bosi huyo wa zamani wa Q Chief aliendelea kufunguka kwa kudai kuwa Q Chief siyo mgeni kwake maana hapo awali aishawahi kuambiwa tabia za msanii huyo kuwa atakuja kumretea fujo kutokana jinsi alivyo.

“Nilijua hili tokea kipindi tunaanza kazi naye pamoja kuwa itafikia wakati tutashindwana kwa tabia zake maana hata watu walinifuata kunieleza sifa zake za ukorofi pia najua haya yatatokea tena kwa wasanii wengine”. Alisema Mhonda

Hata hivyo meneja huyo amesema yote yanayo mtokea siyo sababu ya yeye kuvunjika moyo kushindwa kuwasaidia wasanii.

Q Chillah

“Nimepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni 200 lakini hilo kwa kwangu haliwezi kunivunja moyo kuendelea kuwasaidia vijana wengine”. Alisisitiza Mhonda

Kwa upande mwingine mmiliki huyo aliweza kutoa milioni 1 katika kampeni ya #Namthamini mwanamke kwa kununulia pedi za wanafunzi wa kike ili waweze kutimiza malengo yao kwa wakati.