
Luffa
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Luffa amesema hana tatizo lolote na Quick Racka na sababu kubwa iliyomfanya ahame ni kutokana na kuangalia mwenendo wa maisha yake na kuangalia faida ya maisha yake lakini pia amesema hakuwa na mkataba na Quick hivyo haikumbana kwenye kuondoka.
Hata hivyo Luffa amesema kwa sasa ana mkataba na Wanene ambao haumruhusu kufanya kazi na studio nyingine mpaka mkataba huo utakapokamilika.