
Mlinda mlango wa Misri Essam El Hadary
Kwa hatua hiyo, Misri inakuwa imeweka rekodi ya kuwa taifa pekee liliyotinga fanali mara nyingi zaidi katika michuano, huku likishikilia pia rekodi ya kuwa taifa lililoshinda mara nyingi zaidi kombe hilo, likiwa limeshinda mara 7.
Mlinda lango wa muda mrefu Essam El Hadary alithibitisha ushujaa wake kwa kuokoa penati iliyopigwa na Betrand Traore na kuiwezesha Misri kupata ushindi huo.
Wakati wa muda wa kawaida Mohamed Salah aliiweka kifua mbele Misri baada ya kufunga bao lililosawazishwa na Aristide Bance kwa krosi iliopigwa na Charles Kabore.
Mchezo mwingine wa nusu fainali, utapigwa usiku huu, kati ya Cameroon na Ghana, na mshindi wa mchezo huo, atakutana na Misri, Jumapili Februari 5.