Friday , 20th Jan , 2017

Raundi ya tano ya mechi za kuwania Kombe la Shirikisho l TFF itaanza Jamamosi Januari 21, 2017 kwa timu za Young Africans na Ashanti United kukutana kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, huku Simba ikisubiri hadi Jumapili.

Mashabiki wa Simba na Yanga katika dimba la Taifa

 

Ratiba ya ASFC inaonesha kwamba timu za Alliance na Mbao za Mwanza zitacheza pia keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati Majimaji na Mighty Elephant za Songea zikicheza kwenye Uwanja Majimaji mjini Songea.

Jumapili Januari 22, mwaka huu Ruvu Shooting itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani wakati Toto Africans itacheza na Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Simba itakipiga na Polisi Dar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kadhalika Mbeya Warriors ikicheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Jumatatu Januari 23, mwaka huu Stand United itacheza na Polisi Mara kwenye Uwanja wa Karume Mara wakati Azam itacheza na Cosmopolitan kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Ndanda itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Jumanne Januari 24, mwaka huu Mtibwa Sugar itacheza na Polisi Moro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Kurugenzi ya Iringa itacheza na JKT Ruvu huko Mafinga huku Mbeya City ikipangwa kucheza na Kabela City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya ilihali Madini na Panone zitacheza kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Januari 25, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Singida United na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mchezo mwingine utakaozikutanisha timu za African Lyon na Mshikamano utapangiwa tarehe mpya.