Aidha, taasisi hiyo imesema kuwa tofauti na ambavyo imekuwa ikielezwa kuwa mbu anayesambaza homa ya Dengue huwa anang'ata nyakati za usiku, taasisi hiyo inafahamu juu ya uwepo wa mbu aina ya Aedes Afrikanus ambaye hung'ata wakati wa usiku na ambaye pia husambaza homa ya Dengue.
Mtafiti mwandamizi ambaye pia ni mkuu wa idara ya Malaria na tabia za mbu wa kituo hicho Dkt. Nicodemus Govella, amesema hayo katika mahojiano na East Africa Radio ambapo amesema kwa sasa taasisi hiyo inakusanya pesa kwa ajili ya kufanya utafiti utakaobaini idadi ya mbu wenye ugonjwa huo, maeneo waliyopo, tabia zao na jinsi ambavyo nchi inaweza kukabiliana na ugonjwa huo.