Baadhi ya wanachama wa Simba SC
Kamati ya uchaguzi ya klabu ya simba inataraji kukutana Jumamosi ya wiki hii kuanza kupitia na kufanya uhakiki wa fomu za wagombea zaidi ya 41 waliorejesha fomu za kugombea nafasi mbalimbali.
Jumatatu kamati hiyo itatangaza majina ya wagombea waliopita katika mchujo wa awali na hapo ndipo itakua fulsa ya kupokea mapingamizi kuanzia May 20-22.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Dr. Damas Ndumbalo amesema baada ya mapingamizi hayo kamati itakutana kupitia na kuhoji waliopingwa na waliopinga na baadaye May 30 watafanya usaili.
Baada ya hapo kamati za maadili na rufaa zitaendelea hadi Juni 23 na kuanzia siku inayofuata Juni 24 -28 kampeni zitaanza rasmi.
Ndumbalo ameongeza kuwa muda wa siku tano kwa kampeni ni kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi wa simba na wagombea wanapaswa kuelewa hilo badala ya kulalamika.
Aidha Ndumbalo akaenda mbali zaidi nakutoa onyo kwa mgombea yeyote yule atakayevunja kanuni za uchaguzi kwa kuanza kampeni kabla ya Juni 24 basi atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa kanuni