
Gari ya abiria iliyogongwa na lori
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amesema kuwa ajali hiyo imetokea maeneo ya Ifunda baada ya lori lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kwenda Dar es Salaam kuigonga gari hiyo ya abiria, na kisha kuacha njia na kumgonga mtembea kwa miguu.
Amina Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Masenza amesema madereva wote wamejeruhiwa na wanaendelea na matibabu, huku hali za majeruhi wengine zikiendelea vizuri isipokuwa mmoja ambaye ana hali mbaya hususani ya kifua.
Amesema uchunguzi zaidi kuhusu chanzo halisi ch ajali hiyo unaendelea.
Mashuda wamesema kuwa lori hilo lililokuwa katika mwendo kasi lilikuwa linatokea eneo la Mafinga lilikosa breki na kuigonga hiece hiyo iliyokuwa inatokea Iringa mjini kuelekea kijiji cha Ulete, na kuiburuza umbali wa mita mia moja na pia kumgonga mtembea kwa miguu ambaye alikufa.
Lori lililopata ajali linavyoonekana baada ya ajali hiyo