Maeneo ya Nguji Dodoma
Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho kilichopo umbali wa zaidi ya kilomita 50 kutoka Manispaa ya Dodoma, wamesema miongoni mwa mama wajawazito wamekuwa wakijifungulia porini kutokana umbali wa kuifuata zahanati ya kata iliyopo umbali wa kilomita 13.
Mkunga wa jadi katika eneo hilo Bi. Evelini Lugolein mwenye miaka 80, amesema amefanya kazi ya kuzalisha wanawake wa kijiji hicho kwa muda mrefu na kuzalisha zaidi ya wajawazito 800 kutokana na kijiji hicho kukosa zahanati.
Kaimu Afisa mtendaji wa kata ya hombolo bwawani, daudi kamunya, amesema kijiji hicho ina changamoto kubwa ya huduma ya afya licha ya kuwa na kaya elfu moja mia mbili na ishiriki na nne wakazi zaidi ya elfu nne, lakini pamoja na kupigania kupata zahanati hakuna kilichofanyika.

Godwin Kunambi
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi, amesema suala hilo kwa wanakijiji hao linashughulikiwa na manispaa yake.
Msikilize hapa Daudi Kamunya…Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata



