Wednesday , 16th Nov , 2016

Baraza la Habari Tanzania MCT jana limezindua rasmi mashindano ya umahiri wa uandishi wa habari kwa mwaka 2016 (EJAT 2016) kwa vipengele 19 kushindaniwa.

Kajubi Mukajanga - Katibu Mtendaji MCT

 

Akizungumza katika uzinduzi huo jana jijini Dar es salaam Katibu Mtendaji wa MCT Kajubi Mukajanga alisema mwaka huu kutakuwa na makundi 19 kushindaniwa badala ya 22 kama ilivyokuwa mwaka jana na kuwa limeongezwa kundi jipya la Data Journalism huku kundi la jinsia likiongezewa kipengele cha watoto na wazee.

Mukajanga aliwaomba waandishi wa habari kuanza kuwasilisha kazi zao zilizoandikwa kati ya mwezi Januari mpaka Desemba ambapo sherehe za utoaji wa tuzo hizo zitafanyika Aprili mwakani.