
Donald Trump na Hillary Clinton
Akionekana kwa mara ya kwanza tangu kukiri kushindwa ,mgombea huyo wa chama cha Democrat amesema kuwa ana matumaini kwamba Trump atafanikiwa kuwa Rais wa Wamarekani wote.
Donald Trump atakuwa Rais wa 45 wa Marekani baada ya ushindi mkubwa ambapo atafanya mkutano wake wa kwanza wa mpito na Rais Obama katika ikulu ya White House hii leo.
Bwana Obama alimpongeza mrithi wake katika mazungumzo ya simu mapema asubuhi akisema kwamba siyo siri kwamba yeye na Trump wana tofauti kubwa kati yao.