Tuesday , 8th Nov , 2016

Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC imesema, imeanza kushugulikia tatizo la watu wenye mahitaji maalum kwa kuwaandalia vifaa maalum vya kuwawezesha kushiriki kupiga kura kwa urahisi katika chaguzi zijazo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC Bw. Ramadhani Kailima

.Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo Bw. Ramadhani Kailima ameiambia East Africa Radio kwamba, watahakikisha wanaondoa kasoro zilizojitokeza katika chaguzi zilizopita ili kuwawezesha watu wenye mahitaji maalum kuchagua viongozi wanaowaamini na kupunguza malalamiko ya kuchaguliwa viongozi wasiowataka.

Amesisitiza kwamba, ni haki ya kila Mtanzania anayestahili kupiga kura kufanya hivyo bila vikwazo vyovyote huku akisisitiza jinsi tume hiyo inavyoendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki za mpiga kura bila ubaguzi.