Thursday , 20th Feb , 2014

Rapa Kala Jeremiah ameweka wazi kuwa, kabla hajaamua kuweka nguvu zake zote katika muziki, alikuwa na uwezo mkubwa ya kucheza mchezo wa mpira wa kikapu, ambapo aliweza kujijengea jina kupitia mchezo huo huko Mwanza.

Kala amesema kuwa alikuwa mkali sana wa mchezo huu katika miaka ya 2003 na baada ya kugeukia muziki, kipaji hiki kilipotea na mtazamo wake wa kutoka kimaisha ukabadilika.

Kwa maneno ya Kala mwenyewe, muziki umekatisha ndoto yake ya kucheza katika ligi maarufu zaidi ya mchezo huu duniani NBA, ambayo alikuwa nayo hapo awali.