Tuesday , 11th Oct , 2016

Kampuni ya Vinywaji Baridi ya CocaCola, imejitokeza kuiunga mkono EATV LTD kwenye Tuzo za EATV (EATV AWARDS), ili kuinua sanaa ya Afrika Mashariki.

Afisa Masoko Msaidizi wa CocaCola,Pamela Lugenge (Kulia) akiwa na Meneja Mauzo na Masoko wa EATV LTD, Roy Mbowe.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Pamela Lugenge ambaye ni Afisa Masoko Msaidizi wa CocaCola, amesema wao kama kampuni inayojihusisha na kuinua vipaji kwa vijana, hawakuwa na sababu ya kutounga mkono jambo hilo ambalo ni muhimu na kubwa kwa wasanii wetu, ambao ni mifano bora kwa vijana.

“Kama mnavyojua tuna sababu milioni za kujiamini, kampeni ambayo inahamasisha watu kujiamini katika vipaji vyao na waendelee kuvipigania na kama Copa CocaCola ambayo ni football tournaments, inayovumbua vipaji vya vijana hapa Tanzania”, alisema Pamela

Pamela aliendelea kusema ….................”So, fursa kama hii ya East Africa TV ambayo inawatambua wasanii wetu wa Tanzania na kuwashukuru, kwa vipaji vyao na kuwa role model kwa vijana , sisi hatukuweza kutoshiriki, na kwa kampeni yetu ya mwaka huu ambayo ni onja msisimko, tukaona ni vizuri wakati tunaangalia #EATVAwards, basi tuwe tunajiburudisha na vinywaji vya CocaCola”.

Kampuni ya CocaCoala imekuwa ikiunga mkono mambo mengi ya kuinua vipaji kwa vijana, ikiwemo na mashindano makubwa ya kucheza ya Dancee 100%, ambayo pia yanaendeshwa na EATV LTD.

Tags: