Thursday , 6th Oct , 2016

Msanii AY ambaye tayari ana tuzo 25 tofautofauti kabatini, amezungumzia tuzo kubwa za kwanza Afrika Mashariki zilizoanzishwa na EATV LTD, EATV AWARDS, na kusema ni jambo la neema kwa wasanii.

AY

Akizungumza na eNewz ya East Africa Television, AY amesema mfumo wa tofauti ulioletwa na tuzo hizo wa msanii kujipendekeza mwenyewe, ni mzuri zaidi kwani itamsaidia msanii mwenyewe kujua yeye anafaa wapi zaidi katika kazi zake za muziki.

“Hii ya kujipendekeza katika category flan, inampa mtu mwanga, unajua saa nyingine mtu anawekwa kwenye category ambayo ha'deserve', au mwingine amewekwa katika category ambayo inakuwa kuna makosa mengi, kwa hiyo wewe mwenyewe unavyojipendekeza unaipatia njia lile jopo wakija kufanya selection wanakuwa katika njia bora zaidi”, alisema AY.

AY amesema yeye binafsi ameshachukua fomu za kujipendekeza kushiriki EATV AWARDS, na kilichobaki na wahusika kuamua anafaa au hafai kuingia kwenye nomination ya kupigiwa kura na wananchi.

EATV AWARDS zinahusisha wasanii wote wa filamu na muziki kwa nchi za Afrika Mashariki, na ndizo tuzo kubwa za kwanza kuanzishwa zinazohusisha wasanii wa nchi hizo moja kwa moja.

Tags: