Aika akiwa na Nahreel katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, kilichoruka LIVE kutoka Kawe Dar es Salaam
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio iliyokuwa ikirushwa mmoja kwa moja kutoka Kawe jijini Dar es Salaam, Nahreel amesema tuzo hizo zitaleta heshima kubwa kwenye muziki wa Tanzania, kwani wao kama wasanii wanajivunia kuwa na tuzo za nyumbani.
“Tunawashukuru sana EATV mmetuletea tuzo, kwanza ni kitu kikubwa sana kuwa na tuzo za nyumbani hapa, zinaonesha thamani kubwa sana hasa pale msanii unapopata tuzo za ndani, hata nje tunajisifia sana, tunashukuru na tunafurahi”, alisema Nahreel
Nahreel aliendelea kusema kuwa anatumaini tuzo hizo zitakuwa kubwa zaidi na kuja kubadilisha tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki, kama zilivyo tuzo nyingine kubwa za kimataifa.
EATV AWARDS ndizo tuzo kubwa za kwanza kuanzishwa kwa nchi za Afrika Mashariki, na zitahusisha wasanii wa filamu na muziki wa nchi hizo moja kwa moja, zinazotarajiwa kufikia kilele chake tarehe 10 Desemba 2016.