
Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi.
Mkutano wa mawaziri ulioandaliwa na UNHCR mjini Geneva , umekamilisha hatua ya mwisho ya mchakato wa kina wa mikakati ya suluhu kwa ajili ya wakimbizi wa Rwanda ambao walifungasha virago kati ya mwaka 1959 na 1998, kukimbia machafuko ya kikabila na vita.
Akizungumzia hatua hiyo mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema katika dunia ambayo ina zaidi ya wakimbizi milioni 21, mtazamo usiwe tuu kuwapa ulinzi na msaada wa kibinadamu, lakini katika kusaka suluhu.
Ameongeza kuwa mkutano huo umefikia hatua kubwa ya kutoa suluhu kwa maelfu ya wanyarwanda walioomba hifadhi ya ukimbizi 1959 na 1998 na hivyo kulifikisha ukingoni moja ya tatizo la muda mrefu la wakimbizi barani Afrika.
Washiriki wa mkutano huo wametoka Rwanda na nchi zinazohifadhi wakimbizi hao za Angola, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Kenya, Malawi, Jamhuri ya Congo, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe