Monday , 26th Sep , 2016

Msanii One the Incredible amesema kwa muda mrefu wasanii walikuwa wanahitaji changamoto zitakazosaidia kukuza muziki wao na kuupa heshima, hivyo ujio wa EATV AWARDS ni jambo kubwa kwao.

One the Incredible

Akizungumza na East Africa Radio, One the Incredible amesema EATV AWARDS wasanii walikuwa wanahitaji watu watakaoupa heshima muziki huo, ili uweze kukua zaidi.

"Tunahitaji changamoto hiyo, tunahitaji kuwa na tuzo, tunahitaji kuwa na watu ambao wanahusika katika industry ya muziki, kuweza kutambua au wahusika waweze kutambulika kupitia wanachokifanya, kwa sababu ili muziki uweze kukua inabidi upate heshima kwanza, kwa hiyo hatuwezi tukawa tunafanya tu bila kutambulika heshima ya sanaa iko wapi", alisema One the Incredible

One the incredible aliendelea kusema ....."Ni kitu kizuri ni hatua moja ya ziada ya kwenda kujenga industry iwe katika viwango vizuri zaidi, ni jambo zuri kwa sababu palipo na ushindani siku zote zitakuja na misingi sahihi, pia waongeze vipengele ziwe bab kubwa".

EATV AWARDsS ndizo tuzo kubwa za kwanza Afrika Mashariki zinazohusisha wasanii wa nchi hizo, zilizoanzishwa na EATV Ltd, na zinatarajiwa kufikia kilele chake mwezi Desemba 2016.

Tags: