Monday , 26th Sep , 2016

Msanii Alikiba ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa 'Aje' amesema kuwa tayari yeye amekwisha jisajili kushiriki kwenye tuzo za East Africa Televison zinazofahamika kama EATV AWARDS, ambazo zinatarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu, DSM

Alikiba

Alikiba ambaye alikuwa jaji mwalikwa kwenye fainali za mashindano ya Dance 100% 2016 zilizofanyika siku ya Jumamosi alifunguka na kusema yeye tayari ameshajisajili kushiriki katika tuzo za EATV AWARDS na kusema ni jambo jema lililofanywa na EATV kuweza kutambua thamani ya wasanii na kazi zao za sanaa kwa kuleta tuzo hizo.

"Mimi tayari nimeshajisajili kushiriki tuzo hizo, mimi naona EATV wameonesha jinsi gani wanajali uwepo wa wasanii ambao wanastahili kupata tuzo, ingawa natambua kutakuwa na ushindani mkubwa kutoka katika nchi jirani kama Kenya, Uganda, Burundi lakini niseme tu naamini sisi Tanzania tupo vizuri zaidi si kama naipendelea kwa kuwa ni nchi yangu hapana lakini watu wapo 'Serious' na kazi na kila mtu yupo 'serious' na kitu anachofanya hivyo naamini ushindani ni mkubwa sana" alisema Alikiba

Tags: