Baadhi ya akina mama ntilie wakipika kwa kutumia kuni
Wamesema kuwa hiyo pia itakuwa moja ya njia ya kuwapunguzia mzigo wa gharama kubwa za kutumia nishati ya gesi wakati wa kuandaa vyakula.
Wakizungumza katika mahojiano na Hotmix, akina mama ntilie hao wamesema kwa sasa wanalazimika kutumia mkaa na kuni kama chanzo kikuu cha nishati, kutokana na gharama pamoja na bei kubwa ya gesi, hasa kwa mtumiaji mpya ambaye hushindwa kumudu gharama ya jiko, mtungi pamoja na gesi iliyomo ndani yake.
Akina mama ntilie hao wamesema kuwa iwapo watapatiwa vitendea kazi hiyo, wataweza kupiga hatua kwa kuongeza kipato chao na hivyo kupunguza hali duni ya kifedha inayowakabili idadi kubwa ya akina mama ntilie nchini.