Wednesday , 21st Sep , 2016

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amehutubia mjadala wa wazi wa mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kuwa anafurahia sana mada kuhusu maendeleo endelevu na kubadili maisha, ambayo ndiyo maudhui ya kikao hicho.

ais Yoweri Kaguta Museveni

Amesema mada hiyo imekuja wakati sehemu ndogo ya dunia inafurahia utajiri ilhali maeneo mengi duniani yanaathirika na umaskini.

Hata hivyo amesema kuna nuru kwani bara Afrika lina watu takribani milioni 414 walioondokana na umaskini akisema Uganda mwaka 2004 asilimia 56 walikuwa wanaishi katika umaskini, lakini hivi sasa idadi hiyo ni asilimia 19 na ana matumaini kuwa ifikapo mwaka 2017 itafikia asilimia 10

Kuhusu malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs amesema hatimaye, ajenda ya dunia hivi sasa inagusa viambato ambavyo ni muhimu katika kuleta mabadiliko kwa jamii zilizochochea mapinduzi ya viwanda, hususan kujumuishwa kwa nishati katika orodha ya SDG, kumeondokana na ajenda ya zamani.