Wednesday , 7th May , 2014

Mkuu wa majeshi nchini Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange amesema uimara wa majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC unachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na idara za ukaguzi.

Mkuu wa majeshi nchini Tanzania, Davis Mwamunyange.

Akizungumza mara baada ya kufungua mkutano wa nane wa wakaguzi wakuu wa majeshi ya nchi za SADC unaoendelea jijini Arusha Jenerali Mwamunyange amesema ukaguzi huo unasaidia majeshi hayo kuwa tayari wakati wote.

Mkuu huyo wa majeshi amesema kupitia mikutano ya umoja wa wakaguzi hao wa majeshi ya SADC tayari kumekua na makubaliano ya kuwa na taratibu zinazoshabihiana katika ukaguzi.