Tuzo hizo zitahusisha kazi za muziki na filamu zilizotoka mwaka mmoja uliopita, kuanzia tarehe 1 Julai 2015 mpaka tarehe 30 Juni 2016, na zinazotambulika na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA)
EATV Awards imeanza na vipengele 10 ambavyo ni:-
1. Mwanamuziki bora wa kiume
2.Mwanamuziki bora wa kike
3. Mwanamuziki bora chipukizi
4. Kundi bora la muziki
5. Video bora ya muziki
6.Wimbo bora wa mwaka
Kwa upande wa filamu ni
7. Muigizaji bora wa kiume
8. Muigizaji bora wa kike
9. Filamu bora ya mwaka
Na kipengele cha 10. ni Tuzo ya heshima, ambayo itatolewa kwa mtu aliyetoa mchango wake kwenye sanaa kwa muda wa mwaka mmoja uliopita.